Jumamosi, 23 Desemba 2017



AINA SITA ZA VIZUIZI VINAVYOSABABISHA UMASIKINI WAKO
Watu wengi wanakufa masikini na wanashindwa kufikia mafanikio yao bila wao kujua tatizo ni nini, imekuwa kama ugonjwa watu wengi kuendelea kulalamikia serikali au wazazi wao kuwa wao hawafanikiwi wao ndio sababu,na wengine wamekuwa wakikata tamaa kabisa ya mafanikio yao bila wao kujua nini kinachokwamisha maisha yao kuwa bora. Pamoja na vizuizi vya umasikini mafanikio yako ambapo kama utavifanyia kazi basi utaanza kushuhudia mafanikio katika maisha yako, hakuna aliezaliwa kuwa masikini.
1. Uoga (Fear)
Hichi ni kikwazo kikubwa sana kwa watu wengi katia mafanikio yao, watu wengi wamekuwa masikini na wengine kufa masikini kwasababu ya uoga, uoga wa kukataliwa na uoga wa kushindwa, kama unataka kufanikiwa katika kila kitu kwenye maisha yako usiogope kuomba au kusema chochote mbele ya watu eti kwa kuogopa kukataliwa usiogope, lakini pia usiogope kushindwa yani mtu anataka kufanyabiashara lakini kitu  cha kwanza anawaza ni kushindwa anaamini kuwa yeye hawezi na akianzisha atafeli.  Acha uogo uushinde umasikini kwani uoga wako ndio umasikini wako. “Usiogope”
2. Kukosa msukumo (Lack of agressivenes)
Watu wengi wanashindwa kufanikiwa katika maisha yao kwa sababu ya kukosa msukumo binafsi wa kufanya jambo fulani, hakuna mtu yeyote ambae atakupangia maisha yako au kuna mtu ataacha shughuli zake kwaajili ya kupigania maisha yako, wewe ndio unaejua ugumu na uchungu wa maisha yako, unapaswa kupambana kwa ajili ya maisha yako. Jitume katika kufanya shughuli mbalimbali kwa ajili ya mafanikio yako katika maisha.

3. Ujasiri na kujiamini (Courage and confidance
Watu wengi hawajiamini, Kujiamini ni mwanzo mzuri wa kuthubutu na kuthubutu ndio mwanzo mzuri wa kuelekea katika mafanikio. Jiamini kuwa wewe unaweza na unauwezo ndani yako wa kufanya jambo Fulani, Wakati mwingine acha kusikiliza watu wengine wanasema nini kuhusu uwezo wako wewe usikilize moyo wako na ujifanyie tathmini kabla ya kufanya maamuzi.
 4. Kukosa lengo maalumu (Lack of purpose driven goals)
Je, malengo yako nini? Lengo ni ndoto zenye mipaka, kuna malengo ya muda mfupi, muda mrefu na muda wa kati. Wewe malengo yako ni yapi? hauwezi kufanikiwa katika maisha yako kama huna malengo ya maisha yako. Kama huna malengo panga leo  na uyaandike malengo yako. Mtu asiye na malengo ni sawa na mtu ambae anaenda stendi kupanda gari lakini hajui anaenda wapi.
5. Kutokujitoa (Lak of comittment)
Kujitoa limekuwa tatizo kwa watanzania wengi, ewe mtanzania jitoe kwaajili ya maisha yako acha uvivu wa kufikiria Mungu hashughuliki na wavivu jitoe pambana kwaajili ya maisha yako utafanikiwa. Tunapaswa kujitoa kikamilifu katika shughuli mbalimbali za mafanikio ili tuweze kufikia malengo yetu.
6. Kulinda muda (Time management)
Unatumiaje muda wako?  Wewe kijana wa shule (mwanafunzi) unatumiaje muda wako? Wewe mwalimu unatumiaje muda wako? Wewe mama wa nyumbani unatumiaje muda wako? Ni muhimu kila mtu ajiulize swali hili Je, unatumiaje muda wako?  kila sekunde na saa inayopita lazima uhakikishe unafanya kitu ambacho chenye manufaa kwenye maisha yako, mfano ukitumia masaa mawili unajifunza kitu chenye mafanikio kwenye maisha yako basi unayavuta mafanikio yako masaa mawili kama mafanikio yako yalikuwa uyafikie kwa siku mbili na masaa mawili basi utakuwa umebakisha siku mbili. Watu wengi hususani vijana wanatumia muda wao mwingi sana kuangalia movie “series”, kukaa kijiweni kucheza bao, na kufanya mambo mbalimbali yasiyo na tija katika mafanikio ya kimaisha, hata akina mama na mabinti waliowengi hutumia muda wao mwingi kukaa kuoiga stori za umbea mtaani badala ya kutumia muda wao kufanya mambo ya msingi yenye tija katikam maisha yao.
Kwa mfano; mtu akipoteza masaa mawili kila siku ndani ya mwaka mmoja (siku 366) atakuwa amepoteza jumla ya masaa 732 ambayo ni sawa na siku 30.5 (mwezi mzima). Mtu akipoteza masaa 6 kila siku ni sawa na masaa 2,196 kwa mwaka mzima (siku 366) ambayo ni sawa na siku 91.5 (miezi mitatu). Tunapaswa kujifunza kutunza na kulinda muda tulionao katika kufanya mambo ya msingi katika maisha yetu ya kila siku.

Kwa mawasiliano zaidi na mafunzo zaidi wasiliana nami kupitia 0655950324
Mwl. Msyangi Men Kuruchumila.